SWAHILI MATTERS

by Donovan Lee McGrath

Espen Sørensen aka Mzungu Kichaa


“Mzungu Kichaa” ni nani?
Espen Sørensen, anayejulikana zaidi kwa jina la kisanii Mzungu Kichaa, ni mwanamuziki wa Denmark aliyekulia Tanzania baada ya kuhamia huko na familia yake akiwa na umri wa miaka sita. Akiwa na uwezo wa kuongea Kiswahili kwa wepesi, alijihusisha na muziki wa Bongo Flava na kufanya kazi na studio maarufu ya Bongo Records. Uhusiano wake wa karibu na muziki wa Afrika Mashariki uliwezesha utoaji wa albamu yake ya kwanza, Tuko Pamoja.

Mzungu Kichaa alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kurekodi kwenye Bongo Records mwishoni mwa miaka ya elfu moja mia tisa na tisini pamoja na wanamuziki mashuhuri wa Tanzania kama Juma Nature, Professor Jay na wengine. Katika kipindi hicho alipata jina la utani “Mzungu Kichaa.” Ingawa mwanzoni yeye hakuwa msanii mashuhuri sana, alishiriki kuimba sehemu za kibwagizo katika nyimbo mbalimbali mnamo mwaka elfu mbili na moja.

Baada ya kusoma Muziki na Anthropolojia ya Utamaduni nchini Uingereza na kukamilisha shahada ya uzamili katika masomo ya Afrika, alirejea kwenye shughuli za muziki. Mwaka elfu mbili na sita alianzisha kundi la Effigong, na mwaka elfu mbili na nane akaanza rasmi kazi yake kama msanii pekee. Albamu yake ya kwanza ilitolewa Afrika Mashariki mwaka elfu mbili na tisa, na baadaye ikatolewa Ulaya baada ya kupata nafasi ya kuchezwa kwenye vituo kadhaa vya redio.

Nyimbo za albamu hiyo, zikiwemo “Jitolee” (akimshirikisha Professor Jay) na “Wajanja,” zimeimbwa kwa Kiswahili na zinazungumzia masuala ya kijamii kama vile umaskini nchini Tanzania. Ili aitangaze albamu hiyo, Mzungu Kichaa alifanya ziara ya muziki nchini Tanzania, Kenya na Denmark
mwaka elfu mbili na tisa. Wimbo wake wa “Jitolee” ulipata mafanikio makubwa na ukawa maarufu nchini Tanzania na Kenya.

Who is “Mzungu Kichaa”?
Espen Sørensen, better known as Mzungu Kichaa, is a Danish musician who grew up in Tanzania after moving there with his family at age six. Fluent in Swahili, he became involved in Tanzania’s Bongo Flava music scene and worked with the influential studio Bongo Records. His deep connection to East African music led to the release of his first solo album, Tuko Pamoja.

Mzungu Kichaa was among the early artists recording at Bongo Records in the late 1990s alongside notable Tanzanian musicians such as Juma Nature, Professor Jay, and others. During this period, he earned the nickname “Mzungu Kichaa,” meaning “Crazy White Man.” Although he was not initially a prominent performer, he contributed vocals to several tracks around 2001.

After studying Music and Cultural Anthropology in the UK and completing a master’s degree in African Studies, he returned to music. He formed the group Effigong in 2006 before launching a solo career in 2008. His debut solo album was released in East Africa in 2009 and later in Europe after receiving radio airplay.

The album’s songs, including “Jitolee” (featuring Professor Jay) and “Wajanja,” are performed entirely in Swahili and address social issues such as poverty in Tanzania. To promote the album, Mzungu Kichaa toured Tanzania, Kenya, and Denmark in 2009. His single “Jitolee” became a hit in both Tanzania and Kenya.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.